Selasa, 03 Agustus 2010

Mapishi Part 2: Mandazi




Mandazi ni fav dish yangu katika mfungo, na maharage ya kupaka nakumbuka kwetu bongo, honestly mfungo wa Ramadhani ukifika nakua namiss home kwa sana tuu. Yes mwenyewe naweza kupika lakini ile surrounding ya family and friends ni muhimu specially my father. I am very picky kwenye mandazi, sipendi mandazi yenye nyama ndani namanisha yasio umuka alafu ukipika yanakua ndani yamejaa, napenda andazi liumuke likolee iliki,sukari na nazi. kiufupi napenda mandazi yangu yawe PERFECT.

Vipimo

Unga-7 vikombe
Tui la nazi -1 1/2
Milk-4tale spoons(mimi huwa namixna maziwa, maziwa napasha moto for like 20 seconds then nachanganya na nazi)
Sukari-1cup( depends on how u love sugar on ur mandazi)
Mafuta-3 table spoons
Hamira-2 table spoons
Iliki-3table spoons
Mafuta ya kukaangia

Jinsi ya kutayarisha

Ndani ya bakuli lako kubwa weka unga,sukari,iliki, na mafuta yakiwa bado ya moto
Chukua bakuli lingine weka hamira yote, nazi yako na maziwa,weka kando mpaka hamira ianze kufura
Endelea kuchanganya unga wako kwa vitu ulivyo weka
Mimina hamira ndani ya mchanganyiko wa unga. Changanya na ukande huku ukitumia lile tui la nazi. Tui likipungua unaweza ukaongeza maziwa kwa zaidi. Kanda unga mpaka uwe laini, usiwe mlaini sana na usiwe mgumu sana.
Katika meza weka khanga ama kitambaa, mwagia unga kiduchu ambao utafanya ukiweka mandazi yasishike
Anza kukata madonge yako yaweke kwenye sinia iliyo pakwa unga.
Chukua donge moja, lisukume mpaka uone unatoa mandazi manne, usifanye nene sana wala jembamba sana. Fanya hivyo madonge yote yaishe,
Ukisha maliza, chukua kitambaa kilicho kinene yafinike mandazi yako uyaache yaumuke.
Miye binafsi huwa naayacha kwa muda wa lisaa, sipendi ndani kuwe na nyama so naacha yaumuke mpaaka. Kama unapenda yame na nyama then yaache kwa muda wa dk 30.
Weka karai lako kwenye jiko,mimina mafuta yaache yapate moto, kaanga mandazi mpaka yawe na rangi nzuri, upande moja ukifura geuza mwingine, fanya namna hiyo hadi mandazi yanaisha.

Tidak ada komentar:

Posting Komentar

LinkWithin