Selasa, 03 Agustus 2010

Mapishi: Part 1, Ndizi mbichi


Mliyotaka mapishi na ramadhani inawadia sasa ndio hivyo!, hata mie napenda saaana upishi specially kwenye ramadhani, nimelelewa katika familia kubwa na mwezi wa Ramadhani siku zote inakua ina umuhimu katika familia yetu, kuanzia vyakula mpaka as a family, we get together, we laugh, we cry, we eat and enjoy the holy month of Ramadhan. I am going to share my fav ramadhan dish with you that my beautiful sister used to cook for us( man I miss TZ). Kila bada siku mbili ntakuwa naweka different dish.Leo ntaanza na ndizi mbichi na nyama au utumbo, kama unataka ndizi iwe main course basi ntawapa small dish too, mandazi na maharage ya kupaka. Enjoy.

Vipimo

Ndizi mbichi -20(or more)
Nyama -kil 1( kama unapenda nyama waweza ongeza)
Nazi -2( ya kopo ama kukuna)
Chumvi -kijiko cha sukari
Ndimu -half kionzi
Pilipili mbichi-3
Nyanya ya kopo -3table spoons
Binzari manjano -1 kijiko cha chai
Kitunguu maji -1 Kitunguu thaomu -1 kijiko cha chakula
Tangawizi-1 kijiko cha chakula



Namna ya kupika

Kata nyama ziwe katika cubes
Chemsha nyama,weka chumvi,ndimu na tangawizi
Menya maganda ndizi na uzikate vipande vipande vya kiasi
Zikoshe ndizi na uziweke ndani ya sufuria
Weka maji ndani ya sufuria na uchemshe ndizi zako mpaka ziive
Kata kata vitunguu,nyanya,na uweke binzari
Chemsha ndizi zako mpaka maji yakisha kauka
Miminia supu ya nyama ndani ya ndizi
Wacha vichemke kidogo halafu miminia nazi pili pili na bizari nusu kijiko ndani ya ndizi na uziweke kwenye jiko zichemke mpaka zibakie na urojo kiasi. Onja chumvi na uongeze kadri utakavyopenda.Usisahau pili pili mbuzi.

Tidak ada komentar:

Posting Komentar

LinkWithin