Kusema kweli sijui system ya bongo inafanya kazi vipi kwenye "voice ur opinion". Lakini je wanafunzi wakitaka kuandama ni lazima wafukuzwe kwa mabomu ya machozi?. Mkoani Iringa wanafunzi zaidi ya 10,000 wameandama na kukimbizwa na polisi ambao wanashughulika kutuliza fujo kwa kuwatupia wanafunzi hao mabomu ya machozi. Walichotaka kufanya wanafunzi hao ni kwenda kwa mkuu wa mkoa wa Iringa na kuzisema shida zao, sasa kama wao ni wanafunzi kwanini wasipewe haki yao?. Yeye kama mkuu wa mkoa huo alitakiwa asikilize shida za wanafunzi hao nakujua jinsi ya kuzitatua. Hakuna alojeruhiwa kwa ubaya lakini kumepigwa mabomu kumi au zaidi na wanafunzi wamejeruhiwa kwa miba na vitu vingine.
Kwakweli nchi yangu inanisikitisha sana kwa jinsi inavyo treat elimu na wanafunzi. Hivi raisi wa Tanzania afanye nini aweze ku improve elimu kwa wananchi wake?. Kwanini kila siku wanafunzi hawana haki katika elimu?. Je ni ulimbukeni wa serekali yetu ama ni kudharau sababu watoto wao hawana shida?. Hivi ni haki kwa haya yanofanywa na serekali ya Tanzania?. Katika maisha mnyime mtu vyote lakini usimnyime elimu,kwani ndio itakayo msaidia baadae. Raisi wa Tanzania lazima afanye ya maana katika elimu.
Tidak ada komentar:
Posting Komentar