Selasa, 22 Maret 2011

Msiba mkubwa kwa wapenzi wa Taarab.


Wasanii 13 wa kundi la 5 Star Modern Taarab wamefariki dunia mkoani Morogoro kwa ajali ya gari. Ajali imetokea jana usiku, pande za Mikumi wakiwa njiani kutokea Kyela mkoani Mbeya, baada ya Coaster waliyokua wanasafiria kuligonga lori lililokua limepaki barabarani. Baadhi waliofariki ni pamoja na kinara wa kundi hilo Issa Kijoti(Msitujadili),Sheba Juma,Nassoro Madenge,Husna Mapande,Omary hashimu. Katika majeruhi alikuamo mkongwe wa Taarab nchini bi Mwanahawa Ally. Ajali hii imesababisha maiti kuto tambulika, polisi wa mkoa wa Morogoro wanafanya juu chini ili maiti ziweze tambulika.

Poleni wapenzi wenzangu wa Taarab kwani ni pigo kubwa sana tulopata. Mimi binafsi nlitokea sana kulipenda kundi la 5 Star Modern Taarab na vipaji vyao. M/mungu azilaze roho za marehemu mahala pema peponi. Amin
Msikilize Issa Kijoti enzi za uhai wake.

Tidak ada komentar:

Posting Komentar

LinkWithin