Kamis, 17 Maret 2011

Katika utoto wako ulikua unaogopa nini?.


Mie mwenzenu nlikua naogopa ngongoti, Majambo (muuza karanga) na dawa ya mbuu ( Wale walovaa nguo nyeupe wanapita nyumba kwa nyumba, nlikua nadhani wanyonya damu). Lakini sasa nlikua nkiwaona ngongoti basi ntalia, ntakimbia nitaenda kujificha na sitoki hadi nifatwe. Uwoga mwingine wazimu mtupu lakini sadly hadi kesho nawaogopa ngongoti. Nakumbuka kuna siku nlikua nimekaa barazani na mama basi wakawa wanakuja nikaona jitu refu nlitoka mbio hadi chumbani, sikutoka for atleast 30minutes, nlipotoka chozi hilo. Sijui kwanini lakini wamekaa very weird, urefu,misura na kila kitu. If you really want to mess with me then nipeleke sehemu ilokua na mivitu hii phew i ll pee on pants nawala siwatanii.

Tidak ada komentar:

Posting Komentar

LinkWithin