Rabu, 20 April 2011

Really?


Naombeni mjue sifanyi hii post kumponda mtu ila nafanya hii post kuambizana ukweli. Kuambizana ukweli ni muhimu haswa kwa sisi wanawake kwani tunatumia vipodozi vya kila aina. Nimeweka hizi picha sio kumsema mtu ila kusema yakwamba ukimuona mwenzio anatoka kama hivo mwambie tuu usimfiche. Nimeona picha nyingi za madada wa Kibongo mastar na wasio mastar wakipaka makeup ambazo haziendani na skin tone zao.

Unamkuta mtu dark skin anapaka makeup ya light skin na light skin anapaka ya kizungu kabisa unaishia kua HOTMESS. Either wauza vipodozi wa bongo hawawafanyii justice customer wao au wapakaji hawajui wanacho kifanya. Alafu kwanini mtu unakua unajaribu sana kumatch eyeshadow na nguo,pochi,bangili na hereni ulovaa?. Jamani saa nyingine little is better na too much is just TOO MUCH. Ukiniona nimepaka makeup kama hivo jamani feel free kunimwagia maji.

Tidak ada komentar:

Posting Komentar

LinkWithin